Pata taarifa kuu
BURUNDI-NKURUNZIZA-SIASA

Burundi: Rais Pierre Nkurunziza kulipwa mabilioni ya pesa baada ya kustaafu

Wabunge nchini Burundi juma hili wamepitisha muswada wa sheria ambao utampa kitita kikubwa cha fedha rais anayemaliza muda wake Pierre Nkurunziza ikiwemo nyumba ya kifahari na karibu Dola za Marekani 500,000.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya bunge imekuja ikiwa imesalia miezi minne tu kabla ya nchi hiyo kufanya uchaguzi wake mkuu mwezi Mei ambapo rais Nkurunziza amesema hatogombea.

Mswada huo wa sheria unaeleza kuwa katika kila kipindi cha miaka 7, baada ya rais aliyechaguliwa kidemokrasia kumaliza muhula wake, mbali na marupurupu hayo, kiongozi anayemaliza muhula wake atakuwa na mshahara na faida zingine sawa na makamu wa rais ambaye yuko madarakani.

Waziri wa sheria Aime Laurentine Kanyana, amesema sheria ni vema rais anayemaliza muda wake kuheshimiwa na kukipa heshima kiti cha urais nchini humo.

"Inapendeza kuona rais anayeondoka madarakani akipewa heshima, hili tunafanya kwa raia huyu, wale wanaokuja, na wale waliopita," alisema bungeni.

Hata hivyo, Agathon Rwasa mwanasiasa wa  upinzani anakosoa hatua hiyo ya kutoa kiwango kikubwa cha fedha kwa rais anayeondoka madarakani  na kusema lengo ni kumliwaza rais Nkurunziza ili asipate hamu ya kutaka kuwania tena.

"Pengine chama chake  kimeona kuwa  watumie njia hii ili  asitamani kurejea madarakani  ili asigombee tena, ila kwa hali ya uchumi wa nchi inashtua kidogo kuhusu kiasi hicho, " aliongeza.

Mswada huu pia unaeleza kuwa rais anayeondoka madarakani atakuwa na kinga ya kutoshtakiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.