Pata taarifa kuu
FAO-KENYA-ETHIOPIA-SOMALIA

FAO yaonya kuhusu madhara ya nzige katika mataifa ya Afrika Mashariki

Shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na chakula FAO, limeonya kuhusu madhara makubwa yanayoweza kushuhudiwa kutokana na kuenea kwa wimbi kubwa la nzige ambao tayari wanashambulia mazao na mimea kwenye nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia.  

Wakaazi wa Samburu wanajaribu kufukuzana na kundi la nzige katika kijiji cha Lemasulani, Kaunti ya Samburu, Kenya, Januari 17, 2020.
Wakaazi wa Samburu wanajaribu kufukuzana na kundi la nzige katika kijiji cha Lemasulani, Kaunti ya Samburu, Kenya, Januari 17, 2020. REUTERS/Njeri Mwangi
Matangazo ya kibiashara

FAO kwenye taarifa yake imeonya kuhusu nzige hao kuenea kwenye maeneo zaidi ya nchi za Afrika mashariki na kuongeza kuwa tayari wameacha madhara makubwa katika maeneo ambayo wamepita.

Ripoti za kitaalamu zinaonesha kuwa hali ya hewa ya sasa kwenye nchi nyingi za Afrika Mashariki inachangia nzige hao kuzaliana kwa wingi ambapo inakadiriwa kuwa huenda wakazaliana mara 500 zaidi ifikapo mwezi Juni.

Katika hatua nyingine, serikali ya Kenya inahofia uvamizi huu utaleta madhara zaidi licha ya jitihada zake za kupulizia dawa na huenda taifa la Uganda pia likaathirika.

Wizara ya kilimo imekiri wadudu hao waliovamia majimbo ya kaskazini mashariki mwa Kenya sasa wamesambaa maeneo mengi zaidi na yanazidi kuingia nchini kutoka Ethiopia.

Hivi karibuni ndege moja kutoka Djibouti ililazimika kurejea na kutua Ethiopia kufuatia wadudu hao kuziba uwezo wa kuona wa rubani wakati inapita maeneo ya kaskazini mashariki mwa Kenya.

Wakazi wa Eneo la Isiolo kaskazini mwa Nairobi washikilia chupa lililojaa nzige waharibifu.
Wakazi wa Eneo la Isiolo kaskazini mwa Nairobi washikilia chupa lililojaa nzige waharibifu. RFI/Sébastien Nemeth
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.