Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Polisi nchini Kenya wawakamata washukiwa watano wa ugaidi

media Wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia katika harakati za kupaambana na Al Shabab Reuters/Feisal Omar

Maafisa wa polisi nchini Kenya, wamewakamata watu watano waliokuwa wanashukuwa kutekeleza shambulizi la kigaidi jijini Nairobi, baada ya kupata taarifa muhimu za kijasusi.

Ripoti za polisi zinasema kuwa, washukiwa hao ni wanaume watatu,  na wanawake wawili raia wa Marekani, Somalia na Kenya.

Polisi wanaamini kuwa washukiwa hao walikuwa wanapanga kwenda kutekeleza shambulizi hilo Kaskazini mwa jiji la Nairobi wakilenga kilabu moja ya pombe katika barabara ya Kiambu.

Maafisa wan usalama wameimarisha usalama katika jiji hilo kuu, baada ya washukiwa wa Al Shabab kutoka Somalia hivi karibuni kutekekeleza mashambulizi katika kaunti ya Lamu  pwani ya nchi hiyo na Garissa Kaskazini Mashariki karibu na nchi ya Somalia.

Al Shabab imetishia kulengamalshi ya kenya na Marekani, kutokana na mataifa hayo mawili kuendelea kuwa na wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wapiganaji wake.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana