Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Mahakama ya Ufaransa yatathmini rufaa dhidi ya kufutwa kwa kesi ya mauaji ya Habyarimana

media Eneo ambako ndege ya aliye kuwa rais wa rwanda Juvenal Habyarimana ilipodondokea baada ya kudunguliwa ikiwa angani kwenye uwanja wa Kanombe, mjini Kigali, usiku wa Aprili 6 mwaka 1994 © Getty/Scott Peterson

Mahakama ya Ufaransa tangu Jumatano hii Januari 15 inatathmini rufaa dhidi ya kufutwa kwa mashitaka katika kesi ya shambulio dhidi ya ndege ya rais Juvénal Habyarimana, ambalo lilisababisha kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwezi Aprili 1994.

Kesi kuhusu "mauaji na kula njama katika ushirikiano na kundi la kigaidi" ilifunguliwa nchini Ufaransa mnamo mwaka 1998, kufuatia mashitaka yaliyotolewa na familia za raia wa Ufaransa waliokuwa wafanyakazi wa ndege ya rais iliyodunguliwa kwa kombora mapema Aprili 6, 1994 ikijaribu kutuwa katika uwanja wa ndege kimataifa wa kanombe jijini Kigali, nchini Rwanda.

Katika ndege hiyo alikuwemo rais wa Rwanda

Juvénal Habyarimana na rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira na wasaidizi wao wengine, ambao wote walifariki dunia katika tukio hilo.

Majaji wawili waUfaransa wa kitengo kinachopambana dhidi ya ugaidi waliokuwa wakishughulikia kesi hiyo waliamua kuachana nayo mwaka mmoja uliopita Desemba 21, 2018, "baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha", kwa mujibu wa majaji hao ambao pia wamebaini kuwepo na "hoja zinazopingana na ambazo hazikucunguzwa" kuhusiana na ushahidi uliokusanywa.

Pamoja na rufaa hii iliyoanza kuchunguzwa tangu Januari 15, familia za wahanga zinatumaini angalau ya kuanza tena kwa uchunguzi.

Mawakili wa upande wa mashitaka wanataka hasa kwamba mahakama ya Ufaransa ipate ripoti ya siri ya mwaka 2003 kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai iliyoundwa kwa ajali ya Rwanda . Kitengo cha uchunguzi cha Mahakama ya Rufaa ya Paris kitatoa uamuzi wake katika siku zijazo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana