Pata taarifa kuu
BURUNDI-IWACU-HAKI

Waandishi wa habari 4 wa Gazeti la Iwacu na dereva wao kufungwa miaka 15

Mwendesha mashtaka mkuu wa jamuhuri katika Mkoa wa Bubanza kaskazini Magharibi mwa Burundi ameomba kifungo cha miaka 15 jela dhidi ya waandishi wa habari 4 wa Gazeti la Iwacu na dereva wao wakituhumiwa kile kinachodaiwa kuwa “walishirikiana na waasi kuyumbisha usalama”.

Waandishi wa habari wanne wa gazeti la Iwacu na dereva wao wakiwa mahakamani huko Bubanza, Desemba 30, 2019.
Waandishi wa habari wanne wa gazeti la Iwacu na dereva wao wakiwa mahakamani huko Bubanza, Desemba 30, 2019. Tchandrou Nitanga / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo ilianza miezi miwili iliopita wakati waandishi hao wa habari wa Gazeti la kila siku la Iwacu nchini Burundi walipoelekea Mkoani Bubanza, Kaskazini Magharibi mwa Burundi kabla ya kukamatwa wakiwa na dereva wao ambapo walikuwa wamekwenda kuripoti kuhusu waasi wa Burundi waliokuwa wameingia katika mkoa huo wakitokea Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidmokrasia ya Congo.

Katika mahakama ya Mkoa wa Bubanza, mjadala ulidumu kwa takriban saa mbili. Ili kutetea hoja ya kuendelea kuwashikilia waandishi hao wa habari, naibu mwendesha mashtaka ametumia ujumbe wa mmoja kati ya waandishi hao pale alipokuwa akitania na wenzie kwamba waandishi wa habari wa Iwacu wanakwenda Bubanza kuwasaidia waasi.

Mbali na ombi hilo la kifungo cha miaka 15 jela, mwendesha mashtaka ameomba miaka 20 ya kunyimwa haki za raia dhidi ya waandishi hao wa habari pamoja na dereva wao. Kesi hiyo imewekwa faraghani kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Watuhumiwa hao huenda wakahukumiwa kifungo cha miaka kati ya 10 na maisha. Mawakili wao wanayo matumaini kwamba huenda wateja wao wakaachiwa huru.

Mashirika yanayo tetea haki za binadamu yanaona kuwa mashtaka hayo dhidi ya waandishi wa habari wa Iwacu ni ujumbe tosha kwa waadishi wa habari wakati nchi hiyo ikielekea katika Uchaguzi Mkuu mnamo mwezi Mei 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.