Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Marekani yatishia kuwanyima viza watu wanaotatiza mchakato wa amani Sudani Kusini

media Marekani iliitaka Serikali ya Kenya kuchunguza mali zinazomilikiwa na familia za wasomi kutoka Sudan Kusini, zikiwemo mali za aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir, mali ambazo Marekani inasema viongozi hao wamewekeza nchini Kenya. ALEX MCBRIDE / AFP

Marekani imetoa onyo la kuwanyima viza watu wanaoendelea kuwa kikwazo cha kufanikisha juhudi za kupata amani nchini Sudani Kusini.

Tangazo hili limetolewa na Waziri wa Mambo ya nje Mike Pompeo, ambaye amesema wananchi wa Sudan Kusini wameteseka vya kutosha kutokana na vita na kucheleweshwa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Hata hivyo, Marekani haijatoa orodha ya watu wanaolengwa lakini imesema watu hao na familia zao watawekewa vikwazo.

Mwezi Juni 2018 Marekani iliitaka Serikali ya Kenya kuchunguza mali zinazomilikiwa na familia za wasomi kutoka Sudan Kusini, zikiwemo mali za aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir, mali ambazo Marekani inasema viongozi hao wamewekeza nchini Kenya.

Marekani ilisema inao ushahidi wa kutosha kuonesha namna familia na viongozi wa Sudan Kusini wamekuwa wakiwekeza nchini Kenya kwa kutumia fedha za uma huku wengi wakiwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana