Pata taarifa kuu
RWANDA-QATAR-USIRIKIANO-UCHUMI

Rwanda na Qatar zatia saini kuhusu ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Kigali

Shirika la ndege la Qatar limekubali kuchukua asilimia 60 ya hisa katika ujenzi wa uwanja mpya waa kimataifa waa ndege wa Kigali nchini Rwanda, mradi ambao utagharibu zaidi ya dola bilioni 1.3.

Mji mkuu wa Rwanda, Kigali.
Mji mkuu wa Rwanda, Kigali. RFI/Stéphanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa na bodi ya maendeleo ya Rwanda, imesema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi itakuwa na uwezo wa kukimu zaidi ya abiria milioni 7 kwa mwaka katika mji wa Bugesera, ulioko umbali wa kilometa 25 kusini mwa mji mkuu Kigali.

Bodi hiyo imeongeza kuwa awamu ya pili ya mradi inatarajiwa kukamilika mwaka 2032 na utakuwa na uwezo wa kukimu abiria mara mbili zaidi ya ile ya awali na kufikia watu milioni 14 kwa mwaka.

Waziri wa miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete, amewaambia waandishi wa habari kuwa kampuni itakayojenga uwanja huo bado inatafutwa na kwamba mara kazi itakapoanza, awamu ya kwanza ya mradi itachukua miaka mitano kukamilika.

Makubaliano haya yametiwa saini wakati huu mfalme wa Qatar Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani akiwa ziarani nchini Rwanda ambapo pia atahudhuria utoaji wa tuzo ya mapambano dhidi ya Rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.