Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Maporomoko yaua watu wengi Kaskazini Magharibi mwa Burundi

media Nchi nyingi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Kenya na Burundi, zimeendelea kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Hapa ni katika eneo moja la Kenya mwaka 2007. AFP/Brenda Bannon

Watu zaidi ya 20 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na maporomoko ya mlima yaliyoangukia makazi ya watu katika kijiji cha Nyabundu, tarafani Mugina mkoani Cibitoke Kaskazini Magharibi mwa Burundi.

Kulingana na vyombo vya habari nchini Burundi, mpaka sasa idadi ya watu waliofariki kufuatia maporomoko hayo haijajulikana bado.

Redio Isanganiro imeripoti kuwa watu 24 wamefariki dunia kufuatia maporomoko hayo.

Lakini msemaji wa Wizara ya Usalama Pierre Nkurikiye, amesema hajapata ipoti rasmi ya vilivyoharibiwa na maporomoko hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo.

Taarifa kutoka eneo la Nyabundu zinasema mvua nyingi zilizonyesha usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi zilisababisha maporomoko ya ardhi na kumomonyoka kwa mlima mmoja ulio katika eneo hilo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana