Pata taarifa kuu
TANZANIA BARA-ZANZIBAR-KENYA-UGANDA-SUDANI KUSINI-BURUNDI-CECAFA

Michuano ya taji la Cecafa kwa wanawake kufikia tamati Novemba 25, 2019 nchini Tanzania

Michuano ya kuwania taji la Cecafa kwa wanawake inafikia tamati kesho jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa mchezo wa fainali baina ya Tanzania Bara na Kenya.

Mwanahamisi Omar, mshambuliaji wa Tanzania akichuana na ml;inzi wa Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya taji la Cecafa kwa wanawake inayofanyika Dar es Salaam, Tanzania
Mwanahamisi Omar, mshambuliaji wa Tanzania akichuana na ml;inzi wa Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya taji la Cecafa kwa wanawake inayofanyika Dar es Salaam, Tanzania TFF
Matangazo ya kibiashara

Kenya maarufu Harambee Starlets ilifuzu hatua hiyo baada ya kuishinda Burundi kwa mabao 5-0 ilhali Tanzania Bara ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo walitinga fainali kwa kuinyuka Uganda kwa bao 1-0.

Tanzania Bara maarufu Kilimanjaro Queens ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa mara tatu mfululizo huku Kenya wakinuia kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.

Kocha wa Kenya David Ouma wiki hii aliiambia RFI Kiswahili michezo kuwa kikosi chake kina matumaini makubwa ya kushinda mchezio huo utakaochezw akatika uwanja wa Azam Compl;ex, nje kidogo ya jiji.

Katika hatua nyingine katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amesema Cecafa inanuia kutumia michuano hii kupata timu ya kwanza ya wanawake kushiriki michuano ya kombe kla dunia.

Usikose kusikiliza makala ya Jukwaa la Michezo leo Jumapili Novemba 24 mwaka 2019 ambapo mwanahabari wa RFI Kiswahili, fredrick Nwaka amefanya mahojiano na Katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu soka la wanawake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.