Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Kile Kanisa Katoliki la Juba latarajia kwa ziara ya Papa Francis Sudani Kusini

Siku nane zilizopita, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis alitangaza kwamba atazuru Sudani Kusini mwaka ujao bila kutaja tarehe. Pia amewataka wahusika katika mgogoro wa nchi hiyo kujitenga zaidi na mgawanyiko.

Justin Badi Arama, Askofu Mkuu wa Juba, Sudani Kusini, Novemba 17, 2019.
Justin Badi Arama, Askofu Mkuu wa Juba, Sudani Kusini, Novemba 17, 2019. © Sébastien Nemeth / RF
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Aprili, katika tukio lililoshangaza wengi duniani, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani alipiga magoti na kubusu miguu ya Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, ambao waliwasili Roma kwa ibada ya pamoja.

Kwa mara nyingine, katika misa ya Jumapili, Askofu mkuu wa Juba Justin Badi Arama alizungumzia kuhusu mkataba wa amani ulioafikiwa kati ya pande mbili husika na hoja zilizobaki kuweza kufanyiwa kazi. Pande zilizotia saini mkataba huo wa amani zilikubaliana hadi mwezi Februari mwakani kuwa zimeunda serikali ya umoja.

Askofu mkuu wa Juba amezitaka pande husika kuzingatia majukumu yao. "Tumechoka. Viongozi wetu wanatakiwa waweke mbele mateso yanayowakabili raia wao kabla ya maslahi yao ya kisiasa. Tatizo ni kwamba hawaaminiani, wanakosa nia na utashi wa kisiasa. Rais Kiir anasema hataruhusu Riek Machar kuguswa. Lakini inahitaji ujasiri. Kwa hivyo tunachohitaji sasa ni ziara za mara kwa mara na mikutano na kutangazwa kwa mkutano wa pamoja. Itaonyesha kuwa tayari wameanza kujihusisha na manai ya nchi, na watu wataweza kuwaamini. "

Kanisa Katoliki la Sudani Kusini limekaribisha ziara ya ya Papa nchini humo. Lakini kulingana na kanisa hilo, ziara hiyo haina masharti. "Ni baraka kwetu. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, alitangaza kwamba ikiwa serikali itaundwa, atakuja kutoa baraka zake kwa serikali na raia wa Sudani Kusini. Viongozi wetu wanatakiwa kufanye kila wawezalo. Ziara ya Baba Mtakatifu itatoa msukumo mzuri. Ikiwa serikali hii haitaundwa, Papa Francis hatakuja. Ameonya wazi kuwa hatarejelea yale aliyokwisha sema, " Kanisa Katoliki nchini Sudani Kusini limesea katika taarifa.

Mustakabali wa Sudani Kusini uko mikononi mwa mwa watu wawili, amesema Askofu wa Juba Justin Badi Arama, huku akiwaomba kutosahau kwamba ni raia wa Sudani Kusini, na Mungu, ambao ndio waliwapa madaraka hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.