Pata taarifa kuu
TANZANIA-MOMABSA-KENYA

Mkutano wa siku tatu wa kujadili maadili ya taaluma ya afisa uhusiano na uandishi wa habari watamatika Mombasa

Mkutano wa siku tatu uliolenga kujadili maadili ya taaluma ya uafisa mahusiano na uandishi wa habari umekamilika Mjini Mombasa nchini Kenya. 

Rais na mwanzilishi wa chama cha maofisa  mahusiano Tanzania akichangia wakati wa kongamano la siku tatu lililofanyika Mombasa nchini Kenya
Rais na mwanzilishi wa chama cha maofisa mahusiano Tanzania akichangia wakati wa kongamano la siku tatu lililofanyika Mombasa nchini Kenya prst instagram page
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo uliwakutanisha wataalamu wa fani ya afisa uhusiano na uandishi wa habari kutoka mataifa ya Kenya, Tanzania na mataifa mengine duniani.

Rais na mwanzilishi wa Chama cha maofisa uhusiano Tanzania Loth Makuza ameshiriki mkutano huo ambapo moja ya mafanikio yake ni kusaini kwa makubaliano baina ya chama cha wataalamu wa mahusiano wa Tanzania na Uganda kwa ajili ya kufufua chama cha maofisa mahusiano wa Afrika mashariki.

Aidha mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo inayohusus changamoto za stadi za mawasiliano katika karne ya 21 iliyowasilishwa na Mkurugenzi mkuu wa shirikika la utangazaji la KenyaDr. Naim Bilal Yaseen.

Katika mkutano huo, Kenya ilichukua jukumu la uongozi kwa muda wa mwaka mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.