Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Kipyenga cha kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa chapulizwa Tanzania, upinzani ukiweka msimamo wa kutoshiri uchaguzi

media Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Chama hicho ni miongoni mwa vyama saba vilivyosusa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa BBC

Filimbi ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa imepulizwa ambapo kampeni za uchaguzi huo zinaanza hii leo.

 

Kampeni hizo zinaanza leo na zinatarajiwa kukamilika siku moja kabla ya uchaguzi ambao utafanyika Novemba 24 katika eneo lote la Tanzania Bara.

Hata hivyo uchaguzi huo unafanyika wakati vyama saba vya upinzani vikiwa vimetangaza kususia uchaguzi huo huku kwa madai ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi, vikitoa wito kwa rais wa taifa hilo, John Magufuli kufuta uchaguzi huo.

Vyama vilivyosusa kushiriki uchaguzi huo ni CUF, Chadema, ACT Wazalendo, Chaumma, NLD,UPDP,CCK na NCCR Mageuzi.

Chama lawala cha CCM kupitia katibu wake wa itikadi na uenezi Humphrey Polepole kimesema kitashiriki uchaguzi huo na kuahidi kufanya kampeni za kistaarabu huku kikishutumu vyama vya upinzani kwa kuwa na ajenda ya kususia uchaguzi.

Viongozi wa kitaifa akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wameonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayeleta fujo katika uchaguzi huo.

Hata hivyo vyama vingine vya upinzani kikiwemo TLP vimesema vitashiriki uchaguzi huo.

Kujiondoa kwa vyama vya upinzani kumezua mjadala mpana miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii huku baadhi yakiunga mkono na mengine yakipinga hatua hiyo.

Uchaguzi waserikali za mitaa nvchini Tanzania hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana