Pata taarifa kuu
SUDAN-SUDAN KUSINI-KIIR-MACHAR

Umoja wa Afrika wasema rais Kiir na Machar wana nafasi ya mwisho kuunda serikali

Umoja wa Afrika sasa unasema, viongozi wa Sudan Kusini rais Salva Kiir na kiongozi wa upinzani, Riek Machar, wana nafasi ya mwisho ya kuunda serikali ya pamoja, baada ya kushindwa kufanya hivyo tarehe 12 mwezi Novemba.

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Kusini  Riek Machar na rais  Salva Kiir walipokutana katika Ikulu ya Entebbe Novemba 12 2019
Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Kusini Riek Machar na rais Salva Kiir walipokutana katika Ikulu ya Entebbe Novemba 12 2019 ALEX MCBRIDE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imekuja, baada ya Marekani kutoa onyo kama hili wiki hii, na kusema uvumilivu sasa umefika mwisho.

Rais Kiir na Machar, walikubaliana kuunda serikali hiyo ndani ya siku 100 zijazo, baada ya kukutana nchini Uganda.

Mkuu wa Tume inayohusika na masuala ya amani na usalama Smail Chergui, amesema suala ya kuahirishwa mara kwa mara kwa uundwaji wa serikali hii, halikubaliki tena.

“Naamini kuwa marafiki zetu hapa na Marekani, tunaamini kuwa, hatuwezi kuendelea na mchezo wa suala hili kuendelea kuahirishwa,” alisema.

Tibor Nagy, mwanadiplomasia wa Marekani barani Afrika, amesema nchi yake ina mbinu nyingi ya kutumia, lakini hakusema ni hatua gani Washington DC itachukua.

Rais Salva Kiir na kiongozi wa upinzani Riek Machar walitofautiana mwaka 2013, miaka miwili baada ya uhuru, mzozo ambao umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.