Pata taarifa kuu
BURUNDI-RWASA-SIASA-USALAMA

Agathon Rwasa alaani mpango unaoandaliwa wa kutaka kumuua

Ikiwa ni miezi takribani mitano imesalia kabla ya nchi ya Burundi kufanya uchaguzi wake mkuu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha CNL, Agathon Rwasa amelalamikia kuhusu kile alichosema ni njama za Serikali kutaka kukifuta chama chake.

Kiongozi wa upinzani Burundi Agathon Rwasa ainyooshea kidolea cha lawama Serikali kupanga jama za kutaka kukifuta chama chake.
Kiongozi wa upinzani Burundi Agathon Rwasa ainyooshea kidolea cha lawama Serikali kupanga jama za kutaka kukifuta chama chake. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Mbabe huyo wa zamani wa kivita amesema anazo taarifa kuwa idara za usalama nchini Burundi zinapanga kumzushia uasi kama njia ya kumuua au kumtia mbaroni.

Matamshi yake anayatoa wakati huu wafuasi wa chama hicho wakiripotiwa kushambuliwa, kuuawa na hata ofisi zao kuchomwa moto na watu wasiofahamika.

Taarifa hii imethibitshwa na katibu mkuu wa chama cha CNL, Simon Bizimungu.

“Tunazo taarifa za kweli zinazosema kuwa kuna mpango unaondaliwa katika ngazi ya kitaifa kuhusu kuuawa kwa viongozi wa chama cha CNL na kuwazuia jela baadhi yao. Mpango unawalenga viongozi wa juu wa chama, ikiwa ni pamoja na Agathon Rwansa. Mpango huo unaadaliwa na chama tawala CNDD-FDD na viongozi mbalimbali katika jeshi na polisi”, amesema Simon Bizimungu.

“Mpango huo unalenga kuwapa watu silaha na sare za chama cha CNL, ili waonekane kuwa ni wapiganaji wa chama cha CNL. Mwendesha mashitaka papo hapo atachukuwa hatua ya kukamata viongozi mbalimbali wa chama na kufuta chama cha CNL, huo ndio mpango unaoandaliwa, “ ameongeza Agathon Rwasa.

Hata hivyo Rwasa amesema hana nia yoyote ya kuingia msituni au kutoroka nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.