Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Wakimbizi wa Burundi katika kambi ya Nduta mashakani

media Wakimbizi wa Burundi wakisubiri kuruhusiwa kuingia katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania, Juni 11, 2015. AFP PHOTO/STEPHANIE AGLIETTI

Wakimbizi wa Burundi wanaopewa hifadhi katika kambi ya Nduta, Kaskazini magharibi mwa Tanzania, wanaomba msaada kutoka Umoja wa mataifa kufuatia uamuzi wa serikali ya Tanzania kupiga marufuku kwa masuala yoyote ya kibiashara kufanyika ndani ya kambi hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Serikali ya Tanzania ilichukuwa uamuzi wa kuvunja soko kubwa la wakimbizi hao katika kambi ya Nduta. Masoko haya yanayopatikana katika kambi za wakimbizi kutoka Burundi ni sehemu ya kuwapa kipato wakimbizi hawa na kuwasaidia kwenye matumizi madogo madogo.

Wakimbizi wanasema, kitendo hiki pamoja na kuvunjwa kwa soko lao kubwa mwishoni mwa wiki, ni sehemu ya kuwataka waondoke katika kambi hiyo, na kuwalazimisha kurudi nchini Burundi bila wenyewe kutaka.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR, linasema halijapata taarifa yoyote kuhusiana na hatua hiyo ya serikali ya Tanzania

“Hatuna taarifa yoyote kuhusu kubomolewa kwa soko la wakimbizi la Nduta, lakini hilo haliwezi kuwa suala jipya wala kushangaza”, amesema Dana Hughes, msemaji mkuu wa UNHCR, kwa upande Afrika mashariki.

Wiki iliyopita , UNHCR ilitoa ilitoa taarifa ikilaumu serikali ya Tanzania kwa kuwalazimisha wakimbizi kurudi bila wenyewe kutaka.

Wakimbizi zaidi ya 200,000 kutoka Burundi wanaishi kwa sasa katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli mkoani Kigoma, nchini Tanzania

Wengi wao waliondoka nchini Burundi mwaka 2015 baada ya machafuko ya kisiasa kufuatia hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania muhula wa mitatu katika uongozi wa nchi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana