Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA

Uganda: Mvutano waendelea kati ya mamlaka na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda wako katika mgomo kwa zaidi ya wiki moja wakipinga hatua ya serikali ya kuongeza ada ya masomo. Jana polisi ilitawanya mkutano wao mkuu.

Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda.
Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda. © Wikimedia / Eric Lubega and Elias Tuheretze
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi hao wamepandwa na hasira kutokana na na kile wanachobaini kuwa ni kutoweka kwa kiongozi wa chama chao. Julius Kateregga alikamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana dakika chache tu baada ya kufanya mahojiano kwenye runinga Jumatano (Oktoba 30).

Kwa zaidi ya wiki moja, wanafunzi na vikosi vya usalama wamekuwa wakikabiliana katika Chuo Kikuu cha Makerere, moja ya vyuo vikuu vya kongwe barani Afrika. Wanafunzi wanalaani ongezeko la ada ya masomo, hatua iliyochukuliwa hivi karibuni na viongozi wa chuo kikuu hicho,baada ya kupewa agizo na serikali, ongezeko la kila mwaka la 15% kwa miaka mitano mfululizo.

Viongozi wa chuo kikuu wao, wanabaini kwamba ada ya masomo hijabadilishwa tangu miaka kadhaa iliyopita.

Hali hiyo imeendelea kuzua mjadala mkubwa na kusababisha hali ya sintofahamu katika chuo hicho. Uongozi wa Chuo Kikuu cha Makerere ambao umewataja waandamanaji kama "watumizi wa madawa ya kulevya", umewasambaratisha wengi wao. Wanafunzi tisa wamesimamishwa kwenye chuo hicho na wengine 26 wamepewa onyo, ikiwa ni pamoja na Marion Kirabo, ambaye ni mmoja wa viongozi wa chama cha wanafunzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.