Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Waandishi wa habari wanne wa Gazeti la Iwacu wazuiliwa Bubanza

Waandishi wa habari wanne wa gazeti binafsi la Iwacu nchini Burundi wamekamatwa Jumanne mchana wiki hii walipokuwa katika kazi yao ya kutafuta habari katika mkoa wa Bubanza, Magharibi mwa nchi hiyo.

Askari wa Burundi wakipiga doria karibu na msitu wa Rukoko Septemba 17, 2010.
Askari wa Burundi wakipiga doria karibu na msitu wa Rukoko Septemba 17, 2010. AFP/ESDRAS NKIKUMANA
Matangazo ya kibiashara

Waandishi hao wa habari waliokamatwa ni Christine Kamikazi, Agnès Ndirubusa, Térence Mpozenzi, Egide Harerimana na dereva wao Adolphe Masabarakiza.

Gazeti la Iwacu limethibitisha taarifa hii kwenye ukurasa wake wa Twitter. Gazeti hilo linabaini kwamba waandishi hao wa habari wamekamatwa mchana katika Wilaya ya Musigati, ambapo milio ya risasi ilikuwa ikisikika tangu mapema asubuhi.

Wanahabari hao wamekamatwa na Mkuu wa operesheni za kijeshi katika kanda hiyo ya Magharibi, na kuagizwa wanyang'anywe vifaa vyao vya kazi.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Twitter wa gazeti la Iwacu, viongozi wa mkoa wa Bubanza walipewa taarifa na waandishi hao kwamba watakuwa katika wilaya ya Musigati kwa kazi yao ya kila siku.

Wanahabari hao walikuwa wakitokea katika msitu wa Rukoko, karibu na mpaka na DRC. Hayo yanajiri wakati waasi wenye silaha walionekana leo katika Wilaya za Mpanda, Gihanga na eneo la Mitakataka, mkoani Bubanza. Na tayari mapigano yameripoitwa kati ya waasi hao na vikosi vya ulinzi na usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.