Pata taarifa kuu
BURUNDI-UFARANSA-HAKI

Mahakama ya Nanterre yawahukumu waziri wa zamani wa Burundi na mkewe kifungo cha miaka miwili jela

Mahakama ya jinai ya Nanterre nchini Ufaransa imemhukumu waziri wa zamani wa Burundi na mkewe kifungo cha miaka miwili jela na faini ya yuro 70.000 kwa malipo ya uharibifu kutokana na kumtumia mfanyakazi wa ndani kwa kipindi cha miaka kumi nyumbani kwao, Ville-d'Avray, (Hauts-de-Seine).

Mahakama ya Paris.
Mahakama ya Paris. © CC/Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Gabriel Mpozagara, waziri wa zamani wa haki na Uchumi nchini Burundi, na mkewe Candide Mpozagara, wamekutwa na hatia ya kumpa kazi kwa kulazimisha, mfanyakazi huyo, na kumuweka katika mazingira yasiyokuwa ya heshima.

Methode Sindayigaya, mkulima wa zamani wa Burundi mwenye umri wa miaka 39, aliiambia mahakama jinsi alivyokuwa "mtumwa" wa miaka 10 nyumbani kwa wanandoa hao.

Wawili hao wanashtumiwa usafirishaji haramu wa binadamu. Ofisi ya mashitaka jijini Nanterre inawashtumu wawili hao kumnyanyasa raia huyo wa Burundi kwa miaka kumi kwenye makaazi yao, magharibi mwa Paris.

Methode Sindayigaya ambaye alifanyiwa madhila hayo, aliingia nchini Ufaransa akiandamana na mwanae, huku akibaini kwamba alijaribu kuwaambia wanandoa hao kuwa alipoteza pasipoti yake. Awali Gabriel Mpozagara na mkewe walisema kuwa hawakutaka kumuachilia yende hovyo mitaani. Alikuwa kama "mtoto wa nyumbani, rafiki ambaye wakati mwingine alisaidia na kazi za nyumbani". Alitaka kubaki katika makazi yangu, alisema Gabriel Mpozagara.

Kwa kujitetea mahakamani Methode Sindayigaya ameileza mahakama jinsi, alitumiwa kuhudumia watoto kwa miezi mitatu. Miaka kumi alifanya kazi saa 19 kati ya 24, kulishwa vibaya, makazi duni, na kadhalika, wanasheria wake walisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.