Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Kiongozi wa waasi Riek Machar akataa kujiunga katika serikali mpya Sudan Kusini

media Kiongozi wa waasi Riek Machar amewasili nchini Sudani Kusini mwishoni mwa wiki hii ambapo alikutana kwa mara ya pili tangu mwezi Septemba na Rais Salva Kiir kwa lengo la kuandaa kurudi kwake tarehe 12 Novemba. ALEX MCBRIDE / AFP

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Sudan Kusini Riek Machar amewaambia wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanaozuru Juba, kuwa hatakuwa katika serikali ya pamoja na rais Salva Kiir inayotarajiwa kuundwa kufikia tarehe 12 mwezi Novemba.

Machar amesema yeye na rais Kiir wameshindwa kukubaliana kuhusu namna ya kuliunganisha jeshi linaloomuunga mkono rais Kiir na vikosi vyake, akisema hataki kuiweka nchi yake kwenye mzozo kwa sababu suala hili muhimu halijapatiwa ufumbuzi.

Kushindwa kwa viongozi hawa wawili kuelewana kuhusu suala hili la usalama, kunatishia utekelezwaji wa mkataba wa amani nchini Sudani Kusini.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Machar alirejea jijini Juba kujadiliana na rais Kiir kuhusu suala hili lakini hawakuelewana.

Miezi kadhaa iliyopita, rais Kiir alitishia kuendelea na mpango wa kuunda serikali hiyo na wanasiasa wengine wa upinzani iwapo Machar hatakuwa tayari.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana