Pata taarifa kuu
BURUNDI-CNC-VYOMBO VYA HABARI

Burundi yaonya vyombo vya habari kuhusu uchaguzi wa mwaka 2020

Baraza la kitaifa la kudhibiti mawasiliano nchini Burundi, CNC, mamlaka ya serikali inayosimamia vyombo vya habari nchini humo, inatuhumiwa kujaribu kudhibiti kabisa kazi ya vyombo vya habari wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020.

Maafisa wa polisi mbele ya jengo la Redio RPA, Bujumbura, Aprili 26, 2015.
Maafisa wa polisi mbele ya jengo la Redio RPA, Bujumbura, Aprili 26, 2015. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

CNC ilikuwa ilitoa muda hadi jana Jumapili kwa vyombo viwili vya habari kuwa tayari vimesaini kwenye hati iliyopendekezwa na mamlaka hiyo.

CNC iliwashangaza viongozi wa vyombo vya habari nchini humo siku ya Ijumaa wiki iliyopita kwa kuwataka watie saini mara moja kwenye " Kanuni za Sheria ya Maadili ya vyombo vya habari na Wanahabari wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020", sheria mbayo imewekwa kwa kuwataka kufanya kazi "kitaalam". Viongozi wa vyombo vya habari wamebaini kwamba sheria hiyo imewekwa kabla hawajashirikishwa ili waweze kuchangia kutoa maoni yao.

Viongozi zaidi ya thelathini wa vyombo vya habari nchini Burundi waliitishwa "kubadilishana fikra kwa rasimu ya kanuni ya sheria za maadili" iliyoandaliwa na mamlaka ya serikali, CNC.

Vyombo viwili binafsi ambavyo vinaendelea kufanya kazi nchini Burundi, Redio Isanganiro na gazeti la Iwacu, vimekataa kutia saini kwenye Kanuni hiyo ya Sheria za maadili, lakini mwenyekiti wa CNC, Nestor Bankumukunzi amesema kuwa, sheria hiyo inahusu vyombo vyote vya habari vinavyofanya kazi nchini Burundi ikiwa ni pamoja na vile ambavyo havikutia saini kwenye kanuni hiyo ya sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.