Pata taarifa kuu
TANZANIA-AFRIKA KUSINI-KOREA KUSINI-UTAFITI-COSTECH

Wanasayansi 250 kutoka nchi mbalimbali Duniani kukutana Jijini Dar es salaam

Wanasayansi 250 Kutoka Mataifa mbalimbali Duniani ikiwa ni pamoja na kutoka Barani Afrika wanatarajia kukutana jijini Dar es salaam,nchini Tanzania katika Kongamano la siku tano kujadili tafiti za Kisayansi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu.

Watafiti Vijana wakiwa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania COSTECH jijini Dar es Salaam.
Watafiti Vijana wakiwa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania COSTECH jijini Dar es Salaam. Picha/COSTECH
Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia Kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania COSTECH, Dakta Amos Nungu amesema zaidi ya nchi 16 kutoka Barani Afrika zitashiriki Mkutano huo ambao ni Maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Dunia utakaofanyika Mwaka Ujao nchini Afrika Kusini

    “Tanzania itanufaika na Mkutano huu,kwa sababu tunashirikiana vizuri na taasisi za Utafiti za Kikanda na nchini nyingine Duniani kama Afrika kusini na Korea Kusini kuna tafiti ambazo tunashirikiana.” Alisema Dakta.Ningu

Miongini mwa Wanufaika wa Ushirikiano wa Tafiti za Kisayansi kati ya Tanzania na Afrika Kusini ni Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam, Paulo Onyango aliyefanya utafiti wa kubuni teknolojia inayotumika kwenye simu kwa wavuvi wa Samaki.

02:13

Mbunifu wa Teknolojia ya FISHMOB

Kongamano hilo litalofanyika kati ya Novemba 5 na 11 Mwaka huu likiambana na Maonesho ya Tafiti mbalimbali za Wanasayansi kutoka nchi washiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.