Pata taarifa kuu
TANZANIA-KUMBUKUMBU-AMANI

Watanzania waadhimisha miaka 20 ya kukumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa Julius Nyerere

Nchi ya Tanzania hii leo inaadhimisha miaka 20 ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa hilo mwalimu Julius Kambarege Nyerere ambaye aliaga dunia tarehe 14 mwezi 10 mwaka 1999.

Rais wa kwanza wa Tanzania hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere
Rais wa kwanza wa Tanzania hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere Butiama Gallery/Govt
Matangazo ya kibiashara

Hii leo nchini Tanzania ni siku ya mapumziko, wakati huu ambapo wananchi wametakiwa kuendelea kuyaenzi yale mazuri aliyowaachia hayati baba wa taifa hilo ambaye wakati wa uhai wake alisisitiza suala la amani na Umoja miongoni mwa Watanzania na bara la Afrika.

Watanzania wengi wanamkumbuka baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki Octoba 14 mwaka 1999 ikiwa ni miaka 120 leo. Watanzania wanamuenzi mwalimu kwa mengi ,lakini kuu ni ile falsafa yake ya umoja ambayo ilimpelekea kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.

Mwalimu Nyerere anaheshimiwa na Watanzania wengi kwa uadilifu na moyo wake wa kutumikia kuliko kutumikiwa.

Julius Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika eneo la mashariki mwa Ziwa Victoria na alieshi katika maisha ya kawaida, ambapo baba yake alikuwa kiongozi wa kabila ndogo.

Alianza shule akiwa na umri wa miaka 12 na alisomea taaluma ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. Baada ya kufundisha kwa miaka mitatu alipata ufadhili wa kusomeshwa katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.

Alifundisha Kiingereza, Kiswahili, na historia katika Chuo Kikuu cha jijini Dar es Salaam, na kutokana na mwenendo wake aliochaguliwa kuwa mkuu wa shirika la Tanganyika African Association.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.