Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA-SIASA-HAKI

Burundi: Vijana 4 kutoka chama tawala wahukumiwa kwa mauaji ya mwanasiasa wa upinzani

Vijana wanne kutoka kundi la vijana wa chama tawala, CNDD-FDD nchini Burundi, Imbonerakure, ambao Umoja wa Mataifa umewataja kama wanamgambo, wamehukumiwa kifungo cha maisha kwa mauaji ya mwanasiasa wa upinzani mwezi Agosti mwaka huu,vyanzo vya mahakama vimebaini leo Jumatano.

Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure,  walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3.
Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure, walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3. Desire Nimubona/IRIN/www.irinnews.org
Matangazo ya kibiashara

Hukumu hii, ambayo ni hatua nadra kwa vyombo vya sheria nchini Burundi kutokana na dhulma zinazofanywa na vikosi vinavyoshirikiana na serikali ya Burundi, ilitolewa na mahakama ya Muyinga, mashariki mwa nchi hiyo ambayo inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa tangu Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa mwaka 2015, ambao alishinda kwa kura nyingi na kutawazwa kuwa rais.

Hali ya usalama nchini Burundi inaendelea kudodoroa siku baada ya siku, huku vijana kutoka chama tawala, Imbonerakure, na baadhi ya askari waliokosa nidhamu na maafisa wa idara ya upelelezi (SNR) wakinyooshewa kidole kuhusika na hali hiyo hasa kwa kuwashambulia na kuua wafuasi na wanasiasa wa vyama vya upinzani.

Uchumi wa Burundi unaendelea kuanguka kufuatia vikwazo ilivyowekewa na Umoja wa Ulaya na Marekani kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea kushuhudiwa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo masikini ya ukanda wa Maziwa Makuu, moja ya nchi tano zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.