Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI

Mhubiri wa Kiinjili kutoka Marekani aendelea kuzuiliwa Rwanda

Jeshi la polisi nchini Rwanda linamushikilia Tangu Jumatatu wik hii Greff Schoof, raia wa Marekani ambae ni mmliiki na kiongozi mkuu wa kituo cha radio ya kikristo, kwa kosa la kusabisha uma kukosa utulivu.

Kanisa la Kiinjili, Kigali, Rwanda, mwaka 2014. (Picha ya kumbukumbu)
Kanisa la Kiinjili, Kigali, Rwanda, mwaka 2014. (Picha ya kumbukumbu) © SIMON MAINA / AFP / AFP
Matangazo ya kibiashara

Greff Schoof anayemiliki kituo Amaizing Grace amekamatwa na jeshi la polisi asubuhi Oktoba 7 na kufikishwa kwenye ofisi kuu ya idara ya upelelzi nchini Rwanda (RIB).

Kwa upande wake msemaji wa polisi ya Rwanda Jean Bosco Kabera amesema Greff amekamatwa wakati alikuwa akijiandaa kufanya mkutano na wanahabari akilenga kuishutumu serikali ya Rwanda pasipokuwa na kibali.

Greff amekamatwa akiwa na wanahabari huku akizungumzia kuhusu kesi ya kufungwa kwa kituo cha radio cha Amazing Grace na kanisa lake mwaka mmoja uliyopita kufuatia malalamiko ya wanaharakati wa haki za wanawake, wakishutumu kituo hicho kurusha vipindi vinavyodhalilisha wanawake, kesi ambayo bado iko mahakamani

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.