Pata taarifa kuu
BURUNDI-TANZANIA-UNHCR-WAKIMBIZI-USALAMA

Je wakimbizi wa Burundi Tanzania watarudishwa makwao ?

Tarehe ya kuawarudisha nyumbani wakimbizi kutoka Burundi waishio nchini Tanzania sasa imefika. Wengi wanajiuliza iwapo Serikali ya Tanzania itatekeleza mpango wake wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi hao.

Wakimbizi wa Burundi wakisubiri kuruhusiwa kuingia katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania, Juni 11, 2015.
Wakimbizi wa Burundi wakisubiri kuruhusiwa kuingia katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania, Juni 11, 2015. AFP PHOTO/STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwezi Agosti Serikali ya Tanzania iliagiza wakimbizi kutoka nchini Burundi kurudishwa makwao, na kusema kua hali ya kiusalama katika taifa hilo sasa imeimarika.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola alitangaza kuwa wakimbizi 2,000 watarudishwa Burundi kufikia Oktoba mosi.

Tanzania imekuwa inalinyooshea kidole cha lawama shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR kwamba ndio linakataa wakimbizi hao kurudishwa nchini Burundi.

“Tulipokutana na Mamlaka ya Burundi tuligundua kuwa UNHCR ndio wamekuwa wakikwepa jukumu hilo likisema Burundi haina uwezo wa kuwapokea wakimbizi 2000 kwa wiki'' Waziri Lugola alisema katika mahojiano na BBC.

Tanzania inashikilia kuwa sababu iliyoifanya kuwapatia hadhi ya ukimbizi raia hao wa Burundi kwa sasa hazipo na kwamba ina kila sababu ya kuwataka warudi makwao.

Mvutano kati ya shirika hilo la wakimbizi la Umoja wa mataifa na serikali ya Tanzania kuhusu suala la kuwaregesha makwao wakimbizi wa Burundi umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa sasa.

Mwezi Agosti mwaka mwaka 2017, Serikali ya Tanzania ililipatia shirika la UNHCR siku saba kuanza kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari, ama sivyo serikali ifanye zoezi hilo yenyewe.

Serikali ya Tanzania imesifiwa kwa kuendelea kubeba mzigo huu mkubwa wa wakimbizi lakini zaidi kwa kukubali kutekeleza mkakati wa kimataifa ujulikanao kama Comprehensive Refugee Response.

Ni mkakati uliolenga kutafuta namna endelevu ya kuwasaidia wakimbizi kupata ulinzi na mahitaji mengine ya msingi ya kibinadamu.

Lakini zaidi katika kutafuta namna ya kuwashirikisha wakimbizi hawa katika shughuli mbali mbali za maendeleo katika nchi wanazokimbilia.

Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.