Pata taarifa kuu
KENYA-NAIROBI-JENGO-SHULE

Wanafunzi saba wa shule ya msingi wapoteza maisha baada ya kuangukiwa na darasa jijini Nairobi

Wanafunzi saba wa Shule ya msingi katika mtaa wa Dagoretti jijini Nairobi nchini Kenya, wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta na paa la darasa lao la orofa moja Jumatatu asubuhi.

Eneo la tukio la kuporomoka kwa darasa katika mtaa wa Dagoretii jijini Nairobi nchini Kenya
Eneo la tukio la kuporomoka kwa darasa katika mtaa wa Dagoretii jijini Nairobi nchini Kenya Kenya Red Cross
Matangazo ya kibiashara

Mkasa huo ulitokea wakati wanafunzi hao walipokuwa wameingia darasani wakisubiri kuanzia masomo yao katika Shule hiyo binafsi inayoitwa Precious Talent.

Msemaji wa serikali Cyrus Oguna amesema wanafunzi 57 wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta wanakoendelea kupata matibabu.

“Hadi sasa, tunathibitisha kuwa wanafunzi saba wamepoteza maisha na wengine 57 kujeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu,” amesema.

Mamia ya wakaazi wa mtaa huo na wazazi waliokuwa wa kwanza kufika katika eneo hilo la mkasa walionekana wenye hasira kwa kile walichokisema, maafisa wa serikali ya Kaunti ya Nairobi walichukua muda mrefu kufika katika Shule hiyo kuwaokoa wanafunzi hao.

Imebainika kuwa, ujenzi wa Shule hiyo hakuwa imara kwa sababu zilijengwa kwa vifaa duni vya ujenzi, yakiwemo mabati na mbao.

Shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 800, kutoka mtaa huo wenye watu wanaoishi katika maisha magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.