Pata taarifa kuu
RWANDA-LIBYA-WAHAMIAJI

Wahamiaji wahamishwa kutoka Libya: Rwanda yakaribishwa kwa hatua yake

Hivi karibuni Serikali ya Rwanda, Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR na Muungano wa Afrika, AU walitia saini makubaliano ya kuanza mchakato wa kuhamisha wakimbizi kutoka Libya.

Wahamiaji katika kituo wanakozuiliwa nchini Libya, Desemba 2, 2017.
Wahamiaji katika kituo wanakozuiliwa nchini Libya, Desemba 2, 2017. ©Abdullah DOMA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu mia tano watahamishwa kutoka Libya kwenda Rwanda "katika wiki chache zijazo," Hope Tumukunde Gasatura, Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda katika Umoja wa Afrika AU amebaini katika mkutano na waandishi wa habari mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Rwanda imewapa hifadhi ya ukimbizi raia 150,000 kutoka DRC na Burundi waliotoroka makaazi yao kutokana na kudorora kwa usalama katika maeneo wanakoishi.

"Kundi la kwanza lenye watu 500, kutoka pembe ya Afrika, wataondolewa, wakiwemo watoto na vijana walio hatarini,'' taarifa ya pamoja imeeleza.

Ndege za kuwasafirisha kwa wale walio tayari kwenda Rwanda zinatarajia kuanza safari majuma kadhaa yajayo, ilieleza taarifa hiyo.

Rwanda ilitangaza kutoa hifadhi kwa wahamiaji mwezi Novemba mwaka 2017 baada ya chombo cha habari cha CNN kuonesha video ikiwaonesha wanaume wakipigwa mnada kuuzwa kama wafanyakazi wa mashamba nchini Libya.

Maelfu ya wahamiaji wanaelekea nchini Libya kila mwaka wakijaribu kufanya safari ya hatari kupitia bahari ya Mediterranea kuelekea barani Ulaya- wale wanaoshindwa hukamatwa na mamlaka na kuishia kushikiliwa kwenye vituo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya pamoja, takriban watu 4,700 wanakadiriwa kushikiliwa kwenye maeneo yenye hali mbaya ndani ya vituo hivyo.

Camille Le Coz kutoka taasisi ya sera za uhamiaji, think tank Migration Policy, ameiambia RFI kwamba "Mpango kama huo upo baina ya EU na Niger, ambapo wahamiaji kutoka Libya wanahifadhiwa wakati wakisubiri ruhusa ya kuingia Ulaya."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.