Pata taarifa kuu

Wataalam:Uganda haiwezi kufikia malengo yake kutokana na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa

Watalaam nchini Uganda wanaonya kuwa huenda nchi hiyo ikashindwa kufikia malengo ya mwaka 2040 ya kuwa taifa la kutegemea msaada hadi uchumi wa kati iwapo kiwango cha kuzaliana kitaendelea kushuhudiwa.

Mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Mji mkuu wa Uganda, Kampala. ©Thomas Trutschel/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kufikia mwaka 2040, Uganda imeweka malengo ya uchumi wake kuwa imara na kuwa nchi ya kujitegema kutokana na kuimarika kwa sekta ya mafuta na gesi, utali na kilimo.

Hata hivyo, watalaam wanasema huenda malengo hayo yasifiwekiwe kwa sababu ya idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa, suala ambalo wanasema, linaathiri maendeleo ya kiuchumi.

Watoto Milioni 1.6 huzaliwa kila mwaka nchini Uganda, ikiwa na maana kuwa kila mwanamke nchini Uganda, ana uwezo wa kuwa na watoto watano.

Watalaam wanapendekeza kuwa, kiwango hicho kipunguzwe na kila familia iwe na watoto watatu.

Takwimu za watu nchini Uganda zinaonesha kuwa, asilimia 70 ya watu nchini humo ni watoto na vijana ambao wanawategemea wazazi wao.

Hata hivyo, rais Yoweri Museveni amekuwa akiipuza ripoti hizi za watalaam na kuwataka raia wa Uganda kuendelea kuzaana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.