Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Yoweri Museveni na Paul Kagame waahidi kukomesha mgogoro baina ya nchi zao

media Rais wa Angola Joao Lourenço akizungukwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kusaini makubaliano ya amani ya kumaliza uhasama kati ya Rwanda na Uganda, Agosti 21, 2019. © JOAO DE FATIMA / AFP

Marais wa Rwanda na Uganda wamefikia makubaliano ya kumaliza uhasama ulio kuepo kati ya nchi hizi mbili jirani. Paul Kagame na Yoweri Kaguta Museveni wametia saini mkataba wa amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda.

Sherehe ya kutia saini mkataba huo zimehudhuriwa na marais wa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo, Angola na Congo Brazzaville.

Felix Tshisekedi, João Lourenço na Denis Sassou Ngueso wamefanya kazi kubwa kwa kuwapatanisa wawili hao katika mgogoro huo uliokuwa ukiendelea kati ya Rwanda na Uganda.

Mgogoro kati ya nchi hizi mbili umekuwa ukiendelea kwa miaka mitatu sasa, na umekandamiza maisha ya raia kutoka nchi hizi hasa wale wa mpakani.

Chanzo cha mgogoro

Rwanda imekuwa ikishtumu Uganda kushirikiana na waasi wanaoongozwa na Kayumba Nyamwasa na kundi lake RNC kuhatarisha usalama wake, huku ikinyooshea kidole cha lawama serikali ya Kampala kula njama na waasi hao kwa kuwafunga na kuwatesa raia wake.

Hata hivyo Uganda imekuwa ikishtumu serikali ya Kigali kuwatum abaadhi ya maafisa wake kufanya ujasusi katika aridhi yake.

“Tumekubaliana kumaliza tofauti zetu na tumefikia hatua kubwa ya kutia saiuni mkataba wa amani. Tunahakikishi raia wetu kwamba kuanzia sasa tunajianda kufungua mpaka uliokuwa umefungwa na kushughulikia masuala mengine nyeti, “rais Paul Kagame amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Angola.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana