Pata taarifa kuu
TANZANIA-AJALI-USALAMA

Tanzania: Tume ya kubaini chanzo cha tukio la kulipuka lori la mafuta yaundwa

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa viongozi wa Tanzania, mlipuko wa lori la kubeba mafuta uliotokea siku ya Jumamosi, Agosti 10, katika eneo la Msamvu Mkoani Morogoro, karibu kilomita 200 kutoka Dar es Salaam, uliua watu 71.

Sherehe ya mazishi ya waathiriwa wa waliouawa katika mlipuko wa lori la mafuta Morogoro. Agosti 11, 2019.
Sherehe ya mazishi ya waathiriwa wa waliouawa katika mlipuko wa lori la mafuta Morogoro. Agosti 11, 2019. © REUTERS/Emmanuel Herman
Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema waendesha piki piki ndio walioathirika zaidi na mkasa huo.

Serikali ya Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa na bendera zote zimepandishwa nusu mlingoti.

Tume ya uchunguzi imeundwa ilibaini chanzo cha tukio hilo.

Bado chanzo cha ajali hiyo hakijathibitishwa lakini kuna hofu huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Hata hivyo polisi wanasema watu hao walikuwa wakichota mafuta baada ya lori hilo kupinduka katika bara bara kuu mapema Jumamosi wakati ajali hiyo ilipotokea.

Mazishi ya waathiriwa wa mkasa wa Morogoro yalifanyika jana Jumapili. Miili 53 ilizikwa katika makaburi ya pamoja mkoani Morogoro.

Mlipuko huo wa lori la mafuta Morogoro uliharibu mali nyingi Agosti 10, 2019.
Mlipuko huo wa lori la mafuta Morogoro uliharibu mali nyingi Agosti 10, 2019. REUTERS/Emmanuel Herman
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.