Pata taarifa kuu
TANZANIA-MOROGORO-AJALI-PETROLI

Watu zaidi ya 60 wapoteza maisha nchini Tanzania baada ya trela la petroli kuwaka moto

Watu zaidi ya 60 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa nchini Tanzania baada ya kuungua kwa  moto baada ya kulipuka na kuwaka moto  kwa trela la mafuta lililokuwa limeanguka katika mkoa wa Morogoro, Magharibi mwa jiji kuu la kibiashara la Dar es salaam.

Trela la mafuta lilivyowaka moto mjini Morogoro nchini Tanzania Agosti 10 2019
Trela la mafuta lilivyowaka moto mjini Morogoro nchini Tanzania Agosti 10 2019 PHOTO COURTESY | THE CITIZEN
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imetokea Jumamosi asubuhi na ripoti zinasema kuwa, baada ya trela  hilo la mafuta kuanguka, watu walikimbia kwenda kuchota mafuta aina ya petroli wakati mtu aliyekuwa anavuta sigara kwenda katika eneo hilo la tukio.

Mashuhuda wengine wanasema kuwa moto huo ulisababishwa na mtu aliyekuwa anajaribu kuiba betri la trela hilo.

“Watu 62 wamepoteza maisha na wengine wamejeruhiwa vibaya na wamepelekwa hospitalini kwenda kupata matibabu,” amesema Stephen Kebwe Mkuu wa mkoa wa Morogoro.

Aidha, ameeleza  kuwa idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha ni vijana wanaofanya kazi ya kuendesha bodaboda waliokuwa wamekwenda kuchota mafuta hayo.

Rais wa nchi hiyo John Magufuli amesema amesikitishwa sana na ripoti ya kutokea kwa vifo hivyo.

“Nimeumia sana kusikia idadi ya Wtanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali hii, natoa pole kwa wale wote walioguswa na vifo hivyo,” alisema.

Magufuli pia amewataka wananchi wa taifa hilo, kaucha tabia ya kukimbilia vitu hatari kama mafuta, vilipuzi na kemikali wakati ajali kama hizi zinapotokea.

Kwingineko barani Afrika, mwezi Mei kule nchini Niger, watu 80 walipoteza maisha jijini Niamey baada ya kisa kama hiki kutokea.

Mwaka 2010, watu 292 walipoteza maisha baada ya kutokea kwa ajali kama hii nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku watu wengine 203 wakipoteza maisha katika mji wa Maridi nchini Susan Kusini mwaka 2015.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.