Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UGANDA-SIASA-USALAMA

Sudani Kusini yashtumu Uganda kutaka kuhatarisha usalama wake

Viongozi kutoka Sudan Kusini na Uganda wamefanya mkutano wa pamoja kwenye mji wa Magwi ulioko Sudan Kusini, mkutano uliolenga kujadili vitisho vya kiusalama na changamoto baina ya nchi hizo mbili.

Vikosi vya Ulinzi vya Sudani Kusini, wakati wa mazoezi karibu na Juba, Aprili 26, 2019.
Vikosi vya Ulinzi vya Sudani Kusini, wakati wa mazoezi karibu na Juba, Aprili 26, 2019. REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa jimbo la Torit nchini Sudan Kusini, Alberio Tobiolo Oromo, amesema wanazo taarifa za kiintelijensia kuwa baadhi ya wapiganaji waasi wanaishi kwenye makambi ya wakimbizi nchini Uganda na kutoka huko wamekuwa wakipanga njama za kushambulia nchi yao.

Gavana Oromo amezitaja kambi za Adjumani, Kiryandongo na Lamwo kuwa kitovu cha waasi hao kupanga mashambulizi dhidi ya Serikali ya Juba.

Kauli hii imekuja wakati hali ya usalama nchini Sudani Kusini imeendelea kuwa mashakani, kufuatia vitisho vya makundi ya watu wenye kubebelea silaha nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.