Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Afghanistani itawaachilia huru wanamgambo watatu wa Taliban (rais)
E.A.C

Waziri wa Fedha wa Kenya akamatwa kwa madai ya rushwa

media Henry Rotich (kushoto) anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini. CS Henry K. Rotich/twitter.com

Waziri wa Fedha wa Kenya Henry Rotich na viongozi kadhaa wa wizara ya fedha wamekamatwa Jumatatu hii (Julai 22) kwa madai ya rushwa na udanganyifu kuhusiana na mradi wa ujenzi wa mabwawa mawili wenye thamani ya dola milioni mbili, polisi imetangaza.

"Watuhumiwa wanazuiliwa na wanasubiri kupelekwa mahakamani," mkuu wa polisi ya Kenya George Kinoti ameliambia shirika la Habari la AFP, akiongeza kuwa watuhumiwa hao wamejisalimisha kwa maafisa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma, Noordin Haji, kuomba hapo awali waweze kukamatwa.

"Henry Rotich anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini, " imesema taarifa kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Mashitaka ya umma.

Noordin Haji ameeleza kwamba watashtakiwa kwa "kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi" miongoni mwa mambo mengine.

"Katiba yetu inasisitiza baadhi ya maadili yetu yakiwemo uadilifu… kuyatimiza hususan kwa walio uongozini, " ameongeza Mkurugenzi wa Mashitaka ya umma.

Maafisa wengine walioagizwa kukamatwa na kushtakiwa ni pamoja na katibu mkuu katika wizara ya fedha Kamau Thugge, Dkt Susan Jemutai Koech kutoka wizara ya jumuiya ya Afrika mashariki na mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya maendeleo ya Kerio Valley (KVDA) David Kimosop.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana