Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Maswala ya uchumi ya Facebook na Google ni "tishio" kwa "haki za binadamu", kwa mujibu wa Amnesty International
 • Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.1 kwenye vipimo vya Richter lapiga Kaskazini Magharibi mwa Laos
E.A.C

Mkurugenzi Jamii Forums atunukiwa tuzo ya kimataifa ya kutetea uhuru wa habari duniani

media Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Jamii Forums, Maxence Melo Allafrica.com

Mkurugenzi mtendaji wa tovuti ya Jamii Forums ametajwa kuwa miongoni mwa washindi wa tuzo ya kimataifa ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka 2019.

Tuzo hiyo hutolewa na kamati ya kimataifa kwaajili ya ulinzi wa waandishi wa habari CPJ, atakabidhiwa tuzo hiyo mwezi Novemba nchini Marekani.

Taarifa za kutangazwa kwa Melo zimetolewa jana kupitia tovuti ya CPJ na inakuja miaka 13 tangu kuasisiwa kwa mtandao huo mashuhuri wa lugha ya kiswahili duniani.

Melo ameshinda tuzo hiyo sanjari na Patricia Campos Mello kutoka Brazil, Neha Dixit wa India na Lucia Pineda Ubau na Miguel Mora wanaotoka Nicaragua.

Katika taarifa yake CPJ imesema Melo atatunukiwa tuzo hiyo kutokana na kupigania uhuru wa kujieleza kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Tovuti ya Jamii Forums yenye mamilioni ya wasomaji na washirika wa mijadala mbalimbali imejizolea umaarufu kwa kuibua hoja na matukio mbalimbali yenye maslahi kwa Tanzania na CPJ inasema Melo amekuwa akikabiliwa na vikwazo kadhaa kutokana na ujasiri wa kutetea uhuru wa kujieleza kupitia mitandao ya kijamii.

CPJ inasema mwanaharakati huyo amepanda kizimbani mara 81 tangu mwaka 2017 kutokana na uthubutu wake wa kutetea uhuru wa kujieleza nchini Tanzania.

Tangu kutangazwa kushinda tuzo hiyo maelfu ya watanzania wamemiminika kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, Facebook na instagram kutoa pongezi kwa mwanaharakati huyo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana