Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Serikali ya Kenya yasema hakuna Ebola nchini humo

media Waziri wa afya nchini Kenya Sicily Kariuki (Kushoto) akiwa na watalaam wa Ebola katika uwanja wa ndege wa JomoKenyatta jijini Nairobi Juni 17 2019 twitter.com/sicilykariuki

Serikali ya Kenya imewahakikishia raia wa nchi hiyo na wageni kuwa hakuna maambukizi yoyote ya Ebola yaliyoripotiwa nchini humo.

Hii ni baada ya mwanamke mmoja kulazwa katika Kaunti ya Kericho, baada ya kushukiwa kuwa alikuwa na dalili za Ebola.

Mwanamke huyo alikuwa amesafiri kutoka Malaba katika eneo la mpaka na Uganda, baada ya virusi hivyo  kuripotiwa Magharibi mwa nchi hiyo.

Waziri wa afya nchini humo Sicily Kariuki amesema kuwa baada ya uchunguzi dhidi ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36, imebainika kuwa hakuwa na Ebola.

Hata hivyo, Waziri huyo amesema kuwa mgonjwa huo alikuwa na dalili kama za mgonjwa wa Ebola ambazo ni pamoja na kuumwa kwa kichwa, homa kali na kutapika.

'Watalaam wetu wamemfanyia uchunguzi mgonjwa huyo na imebainika kuwa hakuwa na Ebola, kwa sasa anaendelea vizuri,” alisema.

“Nawahakikishia Wakenya wote na wageni kuwa hatuna hatuna hata kisa kimoja cha Ebola,” ameongeza.

Kenya imechukua tahadhari katka mpaka wake wa Busia na Malaba kuhakiksiha kuwa watu wote wanapimwa kuhakikisha kuwa hawana Ebola.

Ugonjwa wa Ebola, umeendelea kusababisha maafa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo kuanzia mwezi Agosti mwaka 2018, watu 1,400 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 2,000 wakiambukizwa.

Kenya haijawahi kuripoti kisa hata kimoja  cha Ebola.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana