Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
E.A.C

Maafisa nane wa polisi wauawa nchini Kenya baada ya gari lao kukanyaga bomu

media Eneo la Konton, kulikotokea kwa shambulizi kuwalenga maafisa wa polisi nchini Kenya Juni 15 2019 Google Maps

Maafisa nane wa Polisi wameuawa katika kaunti ya Wajir nchini Kenya, karibu na mpaka na nchi ya  Somalia baada ya gari walimokuwa wanasafiria kukanyaga bomu lililotegwa ardhini.

Inspekta Mkuu wa Polisi nchini humo Hilary Mutyambai amethibitisha kutokea kwa mlipuko huo na kusema kuwa waliotekeleza wanatafutwa.

Wakati wa shambulizi hilo, maafisa 11 wa polisi walikuwa ndani  ya gari hilo wakipiga doria katika eneo hilo ambalo limeendelea kushuhudia vitisho vya  usalama kutoka kwa kundi la Al Shabab.

Hata hivyo, kundi la Al Shabab halijajitokeza kudai kuhusika na shambulizi hilo.

Mwezi Juni mwaka 2018, maafisa wengine nane waliuawa baada ya kutokea kwa shambulizi lingine kama hili katika Kaunti hiyo.

Kaunti za Wajir, Mandera na Garissa yameendelea kulengwa na kundi la Al Shabab, huku maafisa wa usalama wakishambuliwa zaidi.

Kenya imeendelea kupata vitisho kutoka kwa kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia, baada ya kutuma jeshi lake nchini humo mwaka 2011 kwenda kupambana na kundi hilo.

Tangu mwaka 2007, kundi la Al Shabab limekuwa likiisumbua serikai ya Mogadishu na Umoja wa Afrika uliamua kutuma kikosi chake cha wanajeshi 20,000 kukabiliana na kundi hilo la kigaidi.

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana