Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

DRC yaomba kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

media Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 13 Juni 2019 ikulu/Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi, amesema nchi yake hivi karibuni imeomba kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.

Nchi ya DRC inapakana na mataifa manne kati ya 6 ambayo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki, ambapo rais Tshisekedi amesema ziara yake nchini Tanzania ni kusisitiza ombi lao ili kurahisisha masuala ya kibiashara.

Rais Tshisekedi amesema kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo kutasaidia kupunguza vikwazo vya kibiashara na kuongeza tija katika ufanyaji biashara baina ya mataifa yao.

Rais Tshisekedi alipokelewa na mwenyeji wake majira ya jioni na kwenda moja kwa moja ikulu ya Dar es Salaam ambapo alikuwa ameandaliwa chakula cha jioni.

Akizingumza kwa kifupi katika dhifa hiyo, rais Magufuli amempongeza kwa mara nyingine kuchaguliwa kwake huku akiahidi kumpa ushirikiano.

Rais Magufuli amesema uhusiano wa nchi hizo mbili ni wakihistoria na kwamba ziara yake imethibitisha hilo.

Kwa upande wake rais Tshisekedi ameishukuru nchi ya Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za upatikanaji wa amani ya kudumu kwenye eneo la mashariki mwa nchi ya DRC.

Tshisekedi alitumia hotuba yake pia kuishukuru Tanzania kwa kutoa wanajeshi wa kulinda amani ambapo aliwataka viongozi wote kusimama kuwakumbuka askari waliopoteza maisha.

Akiwa nchini Tanzania rais Tshisekedi enatembelea bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa sehemu kubwa inatumiwa na nchi yake kupitisha mizigo.
 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana