Pata taarifa kuu
UGANDA-KIKIRISTO-MAHUJAJI

Mahujaji 22 wa Kikristo wajeruhiwa nchini Uganda

Mahujaji 22  wa Wakikiristo, wanatibiwa hospitalini jijini Kampala, baada ya kujeruhiwa wakati wakisukumana katika eneo la kuabudu  la Kanisa Katoliki katika eneo la Namugongo.

Hujaji aliyejeruhiwa katika eneo la Namugongo
Hujaji aliyejeruhiwa katika eneo la Namugongo PHOTO via @UgandaRedCross
Matangazo ya kibiashara

Keneth Kategaya kutoka Shirika la Msalaba mwekundu amesema idadi kubwa ya Mahujaji hao  walipata majeraha kichwani.

Gazeti la The Observer limeripoti kuwa watoto ni miongoni mwa watu walionekana wakijarbu kuokolewa baada ya kutokea kwa janga hilo katika eneo la Namugongo.

Ripoti zaidi zinaeleza kuwa mahujaji wengine zaidi ya 1,000 wamepata  majeraha baada ya kupata changamoto mbalimbali za kiafya baada ya kuvimba kwa miguu, baada ya kutembea kwa muda mrefu.

Kila mwaka, maelfu wa Mahujaji kutoka eneo la Afrika Mashariki na Kati huenda nchini Uganda kwenda kukumbuka mashahidi wa Uganda zaidi ya 40  kutoka dhehebu la Anglikana na Katoliki waliokubali kupoteza maisha kwa ajili ya imani yao ya Kikiristo wakati wa Mfalme Mwanga II aliyekuwa anaongoza Ufalme wa Buganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.