Pata taarifa kuu
UGANDA-RWANDA-SIASA-DIPLOMASIA

Uganda yasema inaendelea kuzungumza na Rwanda kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia

Uganda inasema ina nia ya dhati ya kumaliza mvutano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Rwanda, miezi kadhaa  baada ya kufungwa kwa mpaka wa Gatuna kwa sababu ya mvutano wa kidiplomasia katia ya nchi hizo za Afrika Mashariki.

Rais wa Rwanda  Paul Kagame (lKushoto) na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni (Kulia ) walipokutana tarehe 25 mwezi Machi 2018
Rais wa Rwanda Paul Kagame (lKushoto) na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni (Kulia ) walipokutana tarehe 25 mwezi Machi 2018 Photo: Michele Sibiloni
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Uganda Sam Kutesa amewaambia mabalozi wan nchi za nje jijini Kampala kuwa, serikali nchini humo, imekuwa katika mazungumzo ya mara kwa mara na Rwanda kwa lengo la kupata suluhu ya kudumu.

Aidha, Kutesa ameongeza kuwa, jitihada zaidi zinafanyika ili kutatua changamoto zilizopo kidiplomasia na kuhakikisha kuwa suala hili halipitii katika vyombo vya Habari.

Hata hivyo, Waziri huyo amesema kuwa Kampala ilishangazwa na hatua ya Kigali, kufunga mpaka kwa sababu za kiusalama, kwa madai za kisiasa na hata kuwazuia raia wake kutuzuru Uganda, suala ambalo ameeleza ni hatari kwa maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rwanda imejitetea na kusema iliamua kufunga mpaka wa Katuna kwa sababu ya ukarabati, lakini pia imeishtumu Uganda kwa kuwakamata na kuwazuia raia wanaoishi hapa Uganda bila ya sababu zozote.

Uhusiano huu baridi kati ya Kampala na Kigali, umeendelea kuzua hali ya wasiwasi kati ya wananchi wan chi hizo mbili, ambao wameendelea kushirikiana kwa mambo mengi ya kijamii na biashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.