Pata taarifa kuu
TANZANIA-UISALAMU-AFRIKA

Rais John Magufuli mgeni rasmi mashindano ya kuhifadhi Quran

Mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi Quran yanatarajiwa kutimuwa vumbi Jumapili hii Mei 19 jijini Dar es salaam nchini Tanzania, ambapo jumla ya washiriki 20 kutoka mataifa 18 wanashiriki.

Tanzania's president John Pombe Magufuli in Dar es Salaam, October 30, 2015.
Tanzania's president John Pombe Magufuli in Dar es Salaam, October 30, 2015. REUTERS/Sadi Said
Matangazo ya kibiashara

Mshindi wa mashindano hayo atazawadiwa Milioni 20 za Tanzania.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo taasisi ya Al Hikma Foundation  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais wa Tanzania, John Magufuli ambaye ataongoza viongozi mbalimbali wa serikali na dini katika tukio hilo litakalofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Viongozi wengine wastaafu watakaohudhuria ni rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Ally Hassan Mwinyi ambaye ni mlezi wa mashindano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.