Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-KIIR-MAANDAMANO

Rais Kiir: Sitaruhusu maandamano na mbinu zisizo za kisheria kuniondoa madarakani

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameonya kuwa serikali yake hataivumilia maandamano au mbinu zisizokuwa za kisheria kumshinikiza kuondoka madarakani.

Rais wa Sudan Kusini  Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Wiki mbili zilizopita, vuguvugu linalojiita Red Card Movement, limeanzisha harakati za kumtaka rais Kiir kuondoka madarakani, kuanzia siku ya Alhamisi, tarehe 16.

Maandishi kama #KiirMustGo na #SouthSudanUprising, yamekuwa yakishuhudiwa kwenye mitandao ya kijamii, huku waandaaji wakiwa nje ya nchi hiyo.

Harakati hizi zinatarajiwa kufuata mfano wa hali ilivyokuwa katika nchi jirani ya Sudan, baada ya waandamanaji kuanzia mwezi Desemba mwaka 2018, kuanza kushinikiza kuondoka madarakani kwa rais wa zamani Omar Al Bashir.

“Wale watakaojaribu kuharibu utulivu wa nchi watashughulikiwa,” ameonya rais Kiir.

“Namna ya kuimarisha udhabiti wa Sudan Kusini ni kupitia demokrasia na kupitia Uchaguzi, na hili hatutaacha,” ameongeza rais Kiir.

Sudan Kusini ilijikuta katika vita vya kiraia mwaka 2013 baada ya rais Kiir kumshutumu Makamu wake wa rais Riek Machar kutaka kumwondoa madarakani.

Kiir na Machar wametia saini mkataba wa amani, kuunda serkali ya pamoja lakini imesalia vigumu kutekeleza mkataba huo, huku Machar akisalia kuwa nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.