Mvua zasababisha baadhi ya shughuli kukwama Dar es Salaam
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchiniTanzania (MET) imetoa tahadhari juu ya kuwepo kwa mvua kubwa ambayo itaupiga ukanda wa pwani wa nchi hiyo kwa siku tatu mfululizo kutokea leo Jumatatu Mei 13 mpaka Jumatano Mei 15.
Imechapishwa:
MET pia imetahadharisha kuwa kwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii, ukanda huo wa pwani ya Tanzania utakabiliwa na upepo mkali.
Mvua inayoendelea kunyesha imeathiri huduma ya usafiri wa umma hasa usafiri wa mwendokasi, katika mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam.
Utabiri wa Hali ya Hewa wa siku tano na athari zinazoweza kutokea. Umetolewa leo tarehe 13/05/2019 na Mamlaka ya Hali ya Hewa.#utabiriTZ pic.twitter.com/dmfT85yLRY
Tanzania Met Agency (@tma_services) May 13, 2019
Kampuni ya Mabasi ya mwendo kasi (Udart) imelazimika kusitisha huduma zake za usafiri kwa mabasi yanayotumia barabara kuu ya Morogoro, eneo la Jangwani na barabara ya Kawawa katika Bonde la Mkwajuni kuelekea Morocco.
Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Udart, Deus Bugaywa imeeleza kuwa safari zilizositishwa ni kati ya Kimara -Kivukoni, Kimara - Gerezani, Morocco - Kivukoni na Morocco -Gerezani kuanzia mapema alfajiri ya leo Jumatatu.
Wakaazi wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wamekubwa na adha kubwa ya foleni kutokana na mvua hizo kuharibu ama kuziba baadhi ya barabara muhimu.