Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA-USALAMA

Bobi Wine akabiliwa na mashitaka ya kufanya maandamano kinyume cha sheria

Polisi nchini Uganda inamshikilia tangu Jumatatu wiki hii mwanamuziki na mbunge wa Kyadondo, Robert Kagulani maarufu kama Bobi Wine na tayari amefunguliwa mashtaka.

Robert Kyagulanyi anayefahamika kwa jina maarufu la Bobi Wine ni mkosoaji na mpinzani mkubwa kwa utawala wa rais Yoweri Kaguta Museveni.
Robert Kyagulanyi anayefahamika kwa jina maarufu la Bobi Wine ni mkosoaji na mpinzani mkubwa kwa utawala wa rais Yoweri Kaguta Museveni. AFP PHOTO/Michele SIBILONI
Matangazo ya kibiashara

Bob Wine alipandishwa kizimbani katika mahakama moja jijini Kampala na kusomewa mashtaka ya kuandaa mkutano na kufanya maandamano kinyume cha sheria mwaka 2018 na baadaye kuzuiwa katika Gereza la Luzira.

Mmoja wa wanasheria wa Bob Wine, Asuman Basalirwa amesema mteja wake amekamatwa kwa sababu za kisiasa.

Hata hivyo Serikali kupitia kwa naibu msemaji, Shaaban Bantaliza, anasema Bob Wine pamoja na watu wengine wanaopenda kuandamana bila kufuata sheria hawataachwa na mkono wa sheria.

Bob Wine anatajwa kuwa tishio kwa mustakabali wa siasa za rais Yoweri Kaguta Museveni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.