Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C
EAC

Upinzani waandamwa katika ukanda wa Afrika Mashariki

media Wafuasi wa upinzani wakikutana mbele ya makao makuu ya chama chao Zanzibar, Oktoba 28, baada ya tangazo la kufuta uchaguzi. AFP PHOTO / TONY KARUMBA

Wakati huu mataifa kadhaa ya ukanda wa Afrika Mashariki yakijiandaa kwa uchaguzi mkuu, wadadisi wa mambo wanaona kuwa huenda katika chaguzi zijazo vyama vya upinzani vitakosa ushawishi na nguvu na hata baadhi yao kufa.

Nchi za Tanzania na Burundi zitafanya uchaguzi mkuu mwakani huku Uganda na Kenya zitafuatia mwaka 2021 na 2022 huku Rwanda ikitarajiwa kufanya uchaguzi mwaka 2024.

Wadadisi wengi wanaona upinzani huenda usiambulie chochote katika chaguzi zijazo kutokana na namna viongozi wake wamekuwa wakidhibitiwa na vyombo vya dola.

Nchini Burundi upinzani, hasa chama cha CNL kinachoongozwa na Agathon Rwasa kinaendelea kusakamwa na nguvu za dola, huku wafuasi wake wakiendelea kukamatwa katika maeneo mbalimbali, na wengine kufanyiwa vitisho. Hali hiyo inakuja ikiwa umesailia mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Hivi karibu Mkuu wa polisi katika mkoa wa Muyinga, Kaskazini mashariki mwa Burundi, Jérôme Ntibibogora, alisikika kwenye mitandao ya kijamii akionya wafuasi wa chama cha CNL kuwa watakiona cha mtimakuni au kuuawa kama hawataki kutii amri ya utawala.

Nchini Uganda mwanamuziki maaarufu nchini Uganda na mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi, anayejulikana kwa jina maarufu la Bobi Wine

alikamatwa na vikosi vya usalama ba gari yake kuharibiwa vibaya, akijaribu kuelekea eneo ambako alikuwa anasubiriwa kufunguwa tamasha la muziki lililopigwa marufuku na serikali.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana