Pata taarifa kuu
TANZANIA-MAJANGA YA ASILI

Wakaazi wa baadhi ya maeneo Tanzania watahadharishwa kuhusu kimbunga Kenneth

Watalaam wa hali ya hewa wanasema kimbuga Keneth kinatarajiwa kushuhudiwa Pwani ya nchi ya Msumbiji hivi leo. Mvua kubwa, iliyoambatana na upepo mkali, itashuhudiwa huku maeneo ya Pwani ya Tanzania yakilengwa pia.

Dar es-Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania.
Dar es-Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania. Wikimédia/Muhammad Mahdi Karim
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) kimbunga hicho kinatarajiwa kuongeza nguvu zaidi Alhamisi mchana ambapo kitakuwa kinasafiri kwa kilomita 170 kwa saa na kitakuwa kilomita 150 kutoka pwani ya Mtwara.

TMA imetahadharisha kuwa kimbunga hicho kitaingia nchi kavu na nguvu kubwa ya upepo na mvua, itakayosababisha madhara makubwa kwa maisha ya watu na mali zao.

Raia wa Msumbiji ambao hivi karibuni walikumbwa na kimbunga kingine kilichofahamuika kama Idai, wamehimizwa kuwa macho.

Wakati huo huo nchini Afrika Kusini, watu 60 wamepoteza maisha na mamia kusalia bila maakazi yao kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Mashariki mwa nchi hiyo.

Mafuriko makubwa yamesababisha majengo kuporomoko huku maeneo ya mjiji ya Durban na KwaZulu-Natal yakiathiriwa.

Rais Cyril Ramaphosa amewatembelea waathirika wa mafuriko hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.