Pata taarifa kuu
KENYA-CUBA-AFYA-USALAMA

Vikosi vya Kenya vyaendelea kuwatafuta madaktari wawili kutoka Cuba

Hatima ya madakatari wawili, raia wa Cuba, haijulikani, baada ya kudaiwa kutekwa nyara na watu wanaodaiwa kuwa magaidi wa kundi la wanamgambo wa Kiilsamu la Al Shabab, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Maafisa wa usalama na raia wamesimama karibu na gari ambapo watu wenye silaha waliwateka nyara madaktari wawili, raia wa Cuba, wakati walikuwa wakienda kazini katika Kaunti ya Mandera, Kenya, Aprili 12, 2019.
Maafisa wa usalama na raia wamesimama karibu na gari ambapo watu wenye silaha waliwateka nyara madaktari wawili, raia wa Cuba, wakati walikuwa wakienda kazini katika Kaunti ya Mandera, Kenya, Aprili 12, 2019. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya polisi na jeshi vinaendelea na operesheni ya kuwatafuta madaktari hao.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka polisi ya Kenya, huenda madaktari hao wamevushwa hadi nchi jirani ya Somalia.

Madaktari hao ni miongoni mwa kundi la madaktari zaidi ya mia moja kutoa Cuba waliowasili nchini Kenya kwa ombi la serikali, kufanya, kazi kuziba pengo la uhaba wa madaktari nchini humo.

Msemaji wa polisi ya Kenya Charles Owino amebaini kwamba mlinzi wa madaktari hao aliuawa na watekaji nyara, ambao walitoroka na gari na kuingia nchini Somalia.

Hata hivyo kwa mujibu wa Bw Owino akihojiwa na Sauti ya Amerika ya VOA, gari lililokuwa likitumiwa na madakatari hao limepatikana na dereva wake anahojiwa na polisi.

Madaktari hao walitekwa nyara siku ya Ijumaa Aprili 12, Kaskazini Mashariki mwa Kenya, katika Kaunti ya Mandera, karibu na mpaka wa Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.