Pata taarifa kuu
RWANDA-KAGAME-SIASA-USALAMA

Utawala wa Kagame waendelea kukosolewa

Wakati Rwanda ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari, ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamao wa wastani 800,000 waliuawa mnamo mwaka 1994, utawala wa rais Kagame umeendelea kukosolewa na wapinzani wake.

Rais wa Rwanda Paul Kagame kwenye jukwaa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 25, 2018 (picha ya kumbukumbu).
Rais wa Rwanda Paul Kagame kwenye jukwaa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 25, 2018 (picha ya kumbukumbu). © REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

Rais Paul Kagame madarakani tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari amekandamiza upinzani, kwa mujibu wa wapinzani wake.

Miaka miwili iliyopita, Kagame alichaguliwa tena kuwa rais wa Rwanda kwa 98% kwa muhula wa tatu, dhidi ya wapinzani wa kisiasa kutoka jamii ya Wahutu walio wengi, ambao wamenyamanzishwa, lakini pia kati ya washirika wa zamani wa serikali, ambao wamelazimika kukimbilia uhamishoni.

Mwezi uliopita, rais Paul Kagame alitoa kauli iliyozua utata, wakati aliposema kuwa mauaji ya mmoja wa wapinzani wake, Seth Sendashonga, ziadi ya miaka 20 iliyopita, aliuawa kwa sababu alikuwa amevuka mstari mwekundu.

Seth Sendashonga, waziri wa zamani wa mambo ya ndani, ambaye alihitilafiana na Kagame na kulazimika kutoroka nchi, aliuawa nchini Kenya, ambako alikuwa alikimbilia. Familia yake imeendelea kushutumu serikali ya Kigali kuwa ilihusika katiika mauaji yake.

Tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari, wengi wa wapinzani walifanyiwa vitisho, wengine waliuawa nchini Kenya, Uganda, Ubelgiji, Uingereza na Afrika Kusini.

Miaka mitano iliyopita, uhusiano kati ya Afrika Kusini na Rwanda ulikuwa umedorora baada ya viongozi wa Afrika Kusini kukasirishwa na mauaji ya mshirika wa zamani wa rais Kagame jijini Johannesburg. Kanali Patrick Karegeya, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi ya Rwanda, ambaye pia alihitilafiana na Kagame alikutwa aliuawa katika chumba kimoja cha hoteli jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Hata hivyo serikali ya Rwanda imeendelea kufutilia mbali madai ya kuhusika kwake katika mauaji na vitisho kwa wapinzani wake wa kisiasa. Lakini kwa mara kadhaa rais Kagame amekuwa akitoa kauli zisizoridhisha wapinzani wake. "Mtu yeyote atakayefanya uhaini dhidi ya nchi hii atajutia," alisema Kagame siku chache baadaye baada ya mauaji ya Patrick Karegeya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.