Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Upinzani wauangana kumuangusha Museveni katika uchaguzi wa 2021

media Mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi, anayejulikana kwa jina la Bobi Wine kupitia muziki wa Pop. © AFP

Vyama vitatu vya upinzani nchini Uganda vimetia saini mkataba wa ushirikiano kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao, vikiwa na lengo la kumpata mgombea mmoja kupambana na rais Yoweri Museveni.

Vyama hivyo vilivyotia saini mkataba huo ni pamoja na kile cha DP, kinachoongozwa na Nobert Mao, chama cha People`s Progressive party na chama cha Social Democratic party.

“Sasa tumeungana kwa ushirikiano ikiwa ni pamoja na Alliance for National Transformation, Robert Kyagulanyi (Bobiwine)na people power. Tutakuwa na mgombea mmoja ambae atapeperusha bendera yetu”, amesema Nobert Mao, mmoja wa makada wa chama kimoja cha upinzani kilichoshiriki muungano huo.

Hatua hiyo imesifiwa na Bobi Wine, mwanasiasa kijana nchini Uganda ambaye amepata umaarufu hivi karibuni, huku akibaini kwamba muungano huo wa wapinzani ni tishio kwa rais Museveni.

“Nimefurahi tumeanza kuungana. Kila saini inaonesha Museveni leo hii ataondoka madarakani kwa sababu tuko wengi sana na Museveni hana tena nguvu za kuongoza nchi. Wakiomba nipeperushe bendera ya muungano nitafanya hivyo”, amesema Robert Kyagulanyi

Hata hivyo Mike Mukula, Naibu kiongozi wa chama tawala NRM, amesema muungano huo hauwatishi.

“Si mungano wakutisha, na watu bado wanaona kwakweli rais Museveni bado anazo nguvu, amesimama imara wanampa heshima, huyo Mzee wakazi atashinda kabisa bila wasiwasi”, amesema Mukula.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa muungano huu utakuwa na nguvu zaidi iwapo chama kikuu cha upinzani FDC kitaungana na wengine kuongeza nguvu kutokana na umaarufu wa Kiiza Besigye.

Hii ni mara ya tatu kwa vyama vya upinzani kuungana kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mwaka 2016, kuliundwa muungano uliofahamika kama Democratic Alliance, lakini haukufaulu kuingia Ikulu ya Entebee.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana