Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAREKANI-VYOMBO VYA HABARI

Marekani yatoa wito kwa serikali ya Burundi kufungua matangazo ya BBC na VOA

Wizara ya Mambo ya nje nchini Marekani, imetoa wito kwa serikali ya Burundi, kubadilisha uamuzi wake wa kufungia matangazo ya Shirika la Habari la Sauti ya Amerika (VOA) na BBC.

Utawala wa Pierre Nkurunziza umeendelea kushtumiwa kukandamiza wanahabari na vyombo vya habari. .
Utawala wa Pierre Nkurunziza umeendelea kushtumiwa kukandamiza wanahabari na vyombo vya habari. . AFP/Carl de Souza
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara hiyo Robert Palladino ameitaka serikali nchini humo pia kuwaruhusu wanahabari wanaofanya kazi na mashirika hayo, kuwaacha kufanya kazi yao kwa uhuru kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Burundi imechukua hatua hiyo kwa madai kuwa mashirika hayo ya Kimataifa hayafuati sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari nchini' na 'kukiuka maadili ya kikazi'.sheria za nchi hiyo kuhusu uanahabari.

Inaishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo.

Radio kadhaa za kibinafasi zimeharibiwa na kufungwa nchini humo wakati wa mzozo wa kisiasa ulizuka mnamo 2015, wakati rais Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais alioshinda baadaye.

Tangu hapo, takribani watu 430,000 people, wakiwemo wanasiasa wa upinzani wameitoroka Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.