Pata taarifa kuu
UGANDA-RWANDA-USHIRIKIANO

Museveni ajitetea kuhusu mkutano wake na wapinzani wa Kagame

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amevunja ukimya wake kuhusu madai ya kukutana na mfanyibiashara, raia wa Rwanda Tribert Rujugiro Ayabatwa, ambaye inaelezwa ndiye chanzo cha mvutano kati ya mataifa hayo mawili jirani.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mke wake Jeannette Museveni na Paul Kagame (kulia), Rais wa Rwanda na mke wake Jeannette Kagame katika uwanja wa ndege wa Kigali tarehe 29 Julai 2011.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mke wake Jeannette Museveni na Paul Kagame (kulia), Rais wa Rwanda na mke wake Jeannette Kagame katika uwanja wa ndege wa Kigali tarehe 29 Julai 2011. REUTERS / James Akena
Matangazo ya kibiashara

Kupitia barua aliyomwandikia rais wa Rwanda Paul Kagame, tarehe 10 mwezi huu na kuchapishwa katika Gazeti la serikali New Vision, siku ya Jumanne, rais Museveni ameelezea mazingira aliyokutana na mfanyibishara huyo ambaye Rwanda inasema, yeye na wengine ni waasi wanaopanga kuiangusha serikali yake.

Katika barua hiyo, rais Museveni anamwambia rais Kagame kuwa, alikataa kutoa uungwaji mkono kwa mfanyibiashara huyo, ambaye alikuwa anamwelezea mambo ya ndani ya Rwanda, na akamweleza kuwa msimamo wa Umoja wa Afrika ni kwamba, nchi nyingine haiwezi kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Aidha, Museveni ameeleza kuwa alikutana na mfanyabiashara mwingine Bi.Charlotte Mukankusi ambaye alimwomba msaada baada ya kudai kuwa serikali ya rais Kagame ilikuwa imemuua mume wake.

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa barua hii inaonesha kuwa, kuna zaidi ya mvutano wa masuala ya kibiashara wakati huu ufumbuzi ukiwa bado haujapatikana

Serikali ya Rwanda imekuwa ikiishtumu Uganda kwa kuwapa hifadhi na kuwaunga mkono wafuasi wa vuguvugu la RNC, ambalo Kigali inasema ni maadui wa serikali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.